Isaiah 17:1-6

Neno Dhidi Ya Dameski

1 aNeno kuhusu Dameski: “Tazama, Dameski haitakuwa tena mji
bali itakuwa lundo la magofu.

2 bMiji ya Aroeri itaachwa
na itaachiwa mifugo ambayo italala huko,
bila yeyote wa kuyaogopesha.

3 cMji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu,
nao uweza wa ufalme kutoka Dameski;
mabaki ya Aramu yatakuwa
kama utukufu wa Waisraeli,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.


4 d“Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia,
unono wa mwili wake utadhoofika.

5 e fItakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka
na kuvuna nafaka kwa mikono yake,
kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke
katika Bonde la Warefai.

6 gHata hivyo baadhi ya masazo yatabaki,
kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa,
kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni,
nne au tano katika matawi yazaayo sana,”
asema Bwana, Mungu wa Israeli.

Copyright information for SwhKC